top of page

Mwandishi:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

3 Novemba 2026, 15:48:56

Akromegali (acromegaly)

Akromegali (acromegaly)

Majina mengine: acromegaly (Kiingereza)


Aina ya neno: ugonjwa wa homoni


Maana: kuzidi kwa homoni ya ukuaji (growth hormone) kwa mtu mzima.


Maelezo zaidi


  • Dalili: viatu na pete kubana, uso kubadilika (taya kubwa, pua na midomo minene), jasho jingi, maumivu ya viungo, sauti nzito, kukoroma.

  • Madhara: kisukari, shinikizo la juu la damu, magonjwa ya moyo; uvimbe ukibana neva ya macho, kuona kunapungua pembeni.

  • Kwa watoto (kabla ya kumaliza kukua) hali hii huitwa gigantism – urefu kupita kiasi.

  • Matibabu: upasuaji wa uvimbe wa pituitari, dawa, au mionzi.

Imeandikwa:

29 Oktoba 2026, 16:34:25

bottom of page