top of page
Mwandishi:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
6 Novemba 2026, 12:50:31
Chembe sahani (platelets)
Majina mengine: plateleti; thrombocytes, platelets (Kiingereza)
Aina ya neno: sehemu ya damu
Maana: vipande vya seli vinavyotengenezwa kwenye uboho.
Maelezo zaidi
Kiwango cha kawaida: takribani 150–400 × 10⁹/L kwenye kipimo kamili cha damu (FBP).
Kupungua: malaria, maambukizi ya virusi (mf. dengue), VVU, saratani ya damu, baadhi ya dawa, wengu kuvimba, shinikizo la kifafa cha mimba (Pri-eklampsia) na HELLP.
Kuongezeka: maambukizi, upungufu wa madini chuma, baada ya kuondolewa wengu.
Lini umwone mtaalamu wa afya
Madoa mengi ya damu chini ya ngozi, kutokwa damu fizi au puani bila sababu, au damu kwenye mkojo au kinyesi.
Tazama pia: Madoa madogo ya damu (petechiae), Saratani ya damu (leukaemia)
Imeandikwa:
29 Oktoba 2026, 17:28:03
bottom of page

