top of page

Mwandishi:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

6 Novemba 2026, 12:54:18

Chembe ya moyo (epigastrium)

Chembe ya moyo (epigastrium)

Majina mengine: epigastrium; epigastric pain = maumivu ya chembe ya moyo (Kiingereza)


Aina ya neno: sehemu ya mwili


Maana: sehemu ya juu ya tumbo, katikati chini ya mbavu, juu ya kitovu.


Maelezo zaidi


Maumivu yake: mara nyingi hutokana na tumbo, kiungulia au vidonda vya tumbo, lakini kwa mjamzito yanaweza kuashiria Pri-eklampsia, na kwa wengine shambulio la moyo.


Lini umwone mtaalamu wa afya


Mjamzito mwenye maumivu makali ya chembe ya moyo, au maumivu yanayoenda kifuani na mkononi – nenda hospitali mara moja.


Tazama pia: Shambulio la moyo

Imeandikwa:

6 Novemba 2026, 12:51:41

bottom of page