top of page

Mwandishi:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

3 Novemba 2026, 15:48:56

Cipro (ciprofloxacin)

Cipro (ciprofloxacin)

Majina mengine: ciprofloxacin; Ciproxin


Aina ya neno: jina fupi la dawa


Maana: ciprofloxacin, dawa ya kuua bakteria.


Maelezo zaidi


  • Usiinywe pamoja na maziwa, dawa za kupunguza asidi (antacids), madini ya chuma au zinki – hupunguza ufyonzaji; acha angalau saa 2.

  • Kwa kawaida haitumiki kwa wajawazito na watoto isipokuwa kwa maelekezo maalumu.

  • Acha dawa na umwone mtaalamu ukipata maumivu ya kano (hasa nyuma ya kisigino) au mzio.

  • Itumike kwa cheti cha dawa tu – matumizi yasiyo sahihi huongeza usugu wa bakteria.


Tazama pia: Mwingiliano wa dawa (drug interaction)

Imeandikwa:

29 Oktoba 2026, 16:34:25

bottom of page