top of page

Mwandishi:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

29 Oktoba 2026, 17:11:16

Cortisol kuzidi mwilini (Cushing's syndrome)

Cortisol kuzidi mwilini (Cushing's syndrome)

Majina mengine: ugonjwa kortisoli nyingi; hypercortisolism, Cushing's syndrome (Kiingereza)


Aina ya neno: ugonjwa wa homoni


Maana: ziada ya muda mrefu ya glucocorticoid mwilini.


Maelezo zaidi


  • Dalili: unene wa tumbo na uso wa mviringo, nundu nyuma ya shingo, michirizi ya zambarau tumboni, ngozi nyembamba yenye michubuko, misuli dhaifu, shinikizo la juu la damu, kisukari.

  • Kisababishi cha kawaida ni dawa za steroid (pamoja na krimu za kung'arisha ngozi zenye steroid).

  • Usiache steroid ghafla bila maelekezo – huweza kuleta mshtuko wa tezi ya adrenal.


Tazama pia: Upungufu wa homoni za tezi ya adrenal (adrenal insufficiency)

Imeandikwa:

29 Oktoba 2026, 16:34:25

bottom of page