top of page
Mwandishi:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
29 Oktoba 2026, 17:28:14
Fadhaa (agitation)
Majina mengine: agitation (Kiingereza)
Aina ya neno: dalili
Maana: kuongezeka kwa msisimko wa mwili na hisia.
Maelezo zaidi
Chanzo cha mwili kitafutwe kwanza: sukari kushuka, oksijeni kupungua, homa ya uti wa mgongo, malaria kali, kuweweseka (delirium), kuacha pombe, maumivu, kibofu kujaa.
Kutuliza hali: ongea kwa sauti ya chini, mpe nafasi, punguza kelele na watu, epuka kumbishia; dawa hutolewa na mtaalamu inapohitajika.
Lini umwone mtaalamu wa afya
Fadhaa ya ghafla kwa mzee au mgonjwa, au mtu anayetishia kujiumiza au kuumiza wengine – ni dharura.
Tazama pia: Kuchanganyikiwa kuhusu wakati, mahali au nafsi (disoriyentesheni)
Imeandikwa:
29 Oktoba 2026, 17:28:03
bottom of page

