top of page

Mwandishi:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

29 Oktoba 2026, 17:11:16

Fangasi wa ukeni (vaginal candidiasis)

Fangasi wa ukeni (vaginal candidiasis)

Majina mengine: maambukizi ya fangasi ukeni; maambukizi ya Candida albicans ukeni; vaginal candidiasis, thrush (Kiingereza)


Aina ya neno: ugonjwa


Maana: kuzaliana kupita kiasi kwa fangasi Candida ukeni.


Maelezo zaidi


  • Vihatarishi: antibiotiki, ujauzito, kisukari kisichodhibitiwa, VVU na kinga dhaifu, vidonge vya homoni, kuosha uke kwa sabuni, nguo za ndani za kubana zisizopitisha hewa.

  • Uchafu huwa hauna harufu mbaya (tofauti na vajinosisi ya bakteria na trikomoniasisi).

  • Matibabu: dawa za fangasi za kuingiza ukeni (mf. klotrimazoli) au vidonge (mf. flukonazoli) kwa ushauri wa mtaalamu; wajawazito watumie za ukeni.

  • Fangasi wanaojirudia mara 4 au zaidi kwa mwaka – pima kisukari na VVU.


Lini umwone mtaalamu wa afya


  • Dalili kwa mara ya kwanza, wakati wa ujauzito, zisizopona baada ya dawa, zinazojirudia, au pamoja na homa na maumivu ya tumbo la chini.


Tazama pia: Kutokwa na ute ukeni (vaginal discharge), Vajinosisi ya bakteria (bacterial vaginosis)

Imeandikwa:

29 Oktoba 2026, 16:34:25

bottom of page