top of page
Mwandishi:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
3 Novemba 2026, 15:48:56

Hali kali ya ghafla ya selimundu (sickle cell crisis)
Majina mengine: ugonjwa mkali wa ghafla wa seli mundu; sickle cell crisis (Kiingereza)
Aina ya neno: tatizo la ugonjwa wa selimundu
Maana: kuzidi kwa ghafla kwa ugonjwa wa selimundu.
Maelezo zaidi
Aina: maumivu makali (painful crisis), acute chest syndrome, wengu kujaa damu ghafla, upungufu mkubwa wa damu ghafla, na kiharusi.
Vichocheo: maambukizi, upungufu wa maji mwilini, baridi, uchovu mkubwa, msongo wa mawazo.
Kunywa maji ya kutosha, kujikinga na malaria na maambukizi, na kliniki za mara kwa mara hupunguza matukio.
Lini umwone mtaalamu wa afya
Maumivu makali yasiyopungua kwa dawa za nyumbani, homa, kupumua kwa shida, weupe mkubwa, tumbo kuvimba, au udhaifu wa upande mmoja wa mwili.
Tazama pia: Acute chest syndrome
Imeandikwa:
29 Oktoba 2026, 16:34:25
bottom of page

