top of page

Mwandishi:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

29 Oktoba 2026, 17:11:16

Homoni ya ujauzito (hCG)

Homoni ya ujauzito (hCG)

Majina mengine: human chorionic gonadotropin, hCG, beta-hCG (Kiingereza)


Aina ya neno: homoni / kipimo


Maana: homoni ya kondo la nyuma inayodumisha ujauzito wa mwanzo.


Maelezo zaidi


  • Huanza kuonekana kwenye damu siku 8–11 baada ya kutunga mimba, na kwenye mkojo karibu na siku ya hedhi iliyokosekana.

  • Kiwango kisichopanda vizuri huweza kuashiria mimba nje ya mfuko wa uzazi au kuharibika kwa mimba; kiwango cha juu sana huweza kuashiria mimba ya zabibu au mapacha.

  • Pia hutumika kama kiashiria cha baadhi ya saratani (mf. za korodani).


Tazama pia: Umri wa mimba (gestational age)

Imeandikwa:

29 Oktoba 2026, 16:34:25

bottom of page