top of page
Mwandishi:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
29 Oktoba 2026, 17:28:16
Kiharusi cha kuziba kwa mshipa wa damu (ischaemic stroke)
Majina mengine: ischaemic stroke (Kiingereza)
Aina ya neno: ugonjwa / dharura
Maana: kufa kwa tishu za ubongo kwa kukosa damu.
Maelezo zaidi
Dalili (FAST): uso kupinda, mkono au mguu kulegea upande mmoja, maneno kukwama – muda ni ubongo, piga simu ya dharura.
Vihatarishi: shinikizo la juu la damu, kisukari, lehemu nyingi, sigara, mapigo ya moyo yasiyo na mpangilio, selimundu.
CT ya kichwa hutofautisha na kiharusi cha kuvuja damu kabla ya kutoa dawa za kuyeyusha bonge.
Kinga ya kujirudia: aspirini, kudhibiti shinikizo, sukari na lehemu, kuacha sigara.
Lini umwone mtaalamu wa afya
Dalili zozote za kiharusi – nenda hospitali mara moja.
Tazama pia: Kiharusi cha mpito (TIA), Kiharusi cha kuvuja damu (haemorrhagic stroke)
Imeandikwa:
29 Oktoba 2026, 17:28:03
bottom of page

