top of page
Mwandishi:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
29 Oktoba 2026, 17:28:15
Kupasuka kwa utando kabla ya uchungu (PROM)
Majina mengine: chupa kupasuka mapema; PROM, PPROM (Kiingereza)
Aina ya neno: hali ya uzazi
Maana: kupasuka kwa utando wa amnioni kabla ya mikazo ya uchungu.
Maelezo zaidi
Maji hutoka ukeni kwa ghafla au kidogo kidogo na huendelea kutoka.
Mama asiweke chochote ukeni; aende kituo cha afya mara moja.
Hospitalini: kuthibitisha, kuangalia dalili za maambukizi, antibiotiki, steroidi kwa mimba changa, na kuamua wakati wa kujifungua.
Lini umwone mtaalamu wa afya
Maji kutoka ukeni wakati wowote wa ujauzito – hasa yakiwa na harufu, rangi ya kijani au pamoja na homa.
Tazama pia: Maji ya chupa ya uzazi (amniotic fluid), Kuzaliwa kabla ya wakati (njiti)
Imeandikwa:
29 Oktoba 2026, 17:28:03
bottom of page

