Mwandishi:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
8 Novemba 2026, 11:56:45
Kupooza kwa neva ya uso (Bell's palsy)
Majina mengine: kupooza kwa nevafuvu ya saba; facial nerve palsy, Bell's palsy (Kiingereza)
Aina ya neno: ugonjwa wa neva
Maana: udhaifu wa ghafla wa uso upande mmoja bila sababu nyingine inayojulikana.
Maelezo zaidi
Dalili: mdomo kulegea upande mmoja, kushindwa kufunga jicho, kushindwa kutabasamu au kukunja paji la uso upande huo, machozi au mate kutiririka, ladha kupungua.
Hutibiwa kwa prednisolone ikianza ndani ya saa 72; linda jicho kwa matone, mafuta na kulifunga usiku.
Kiharusi hutofautiana: kwa kawaida paji la uso halipooi na huwa na udhaifu wa mkono au mguu.
Lini umwone mtaalamu wa afya
Udhaifu wa uso pamoja na udhaifu wa mkono/mguu, kuongea kwa shida au kizunguzungu – ni dharura (huenda ni kiharusi).
Uso kupooza: mwone mtaalamu ndani ya siku 3 za kwanza.
Tazama pia: Kiashiria cha Bell (Bell's sign)
Imeandikwa:
29 Oktoba 2026, 16:34:25

