top of page
Mwandishi:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
29 Oktoba 2026, 17:28:15
Kutapika kupita kiasi wakati wa ujauzito (hyperemesis gravidarum)
Majina mengine: hyperemesis gravidarum (Kiingereza)
Aina ya neno: ugonjwa wa ujauzito
Maana: kutapika kukali kwa ujauzito chenye upungufu wa maji au kupungua uzito zaidi ya asilimia 5.
Maelezo zaidi
Huanza miezi ya mwanzo (wiki 6–12) na kwa wengi hupungua kufikia wiki 20.
Huwapata zaidi wenye mimba ya mapacha au mimba zabibu – ultrasound hufanyika.
Hutibiwa kwa maji ya dripu, dawa za kuzuia kutapika salama kwa ujauzito, na vitamini B1 (thiamine).
Lini umwone mtaalamu wa afya
Kushindwa kunywa chochote kwa saa 24, mkojo mweusi au kidogo, kizunguzungu, damu kwenye matapishi au kupungua uzito.
Tazama pia: Ujauzito (pregnancy), Kutapika (vomiting)
Imeandikwa:
29 Oktoba 2026, 17:28:03
bottom of page

