Mwandishi:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
29 Oktoba 2026, 17:11:16
Kuvimba kwa kujaa maji (idima)
Majina mengine: idima; edema, oedema (Kiingereza); uvimbe maji; mkusanyiko wa maji kwenye tishu
Aina ya neno: dalili / kiashiria
Maana: mkusanyiko usio wa kawaida wa maji kwenye tishu.
Maelezo zaidi
Aina: ya kubonyea (pitting – kidole kikibonyeza huacha shimo) na isiyobonyea.
Visababishi: moyo kushindwa kufanya kazi, ugonjwa wa figo (nephrotic syndrome), ini kusinyaa, utapiamlo (kwashiorkor), damu kuganda kwenye mshipa wa mguu, mzio, ujauzito, baadhi ya dawa.
Idima ya miguu yote miwili mara nyingi ni ya mwili mzima; ya mguu mmoja huashiria tatizo la mguu huo (mf. DVT).
Lini umwone mtaalamu wa afya
Idima ya ghafla ya mguu mmoja wenye maumivu, uso kuvimba ghafla, au pamoja na kupumua kwa shida – ni dharura.
Mjamzito mwenye uso/mikono kuvimba pamoja na maumivu ya kichwa au kuona ukungu – huenda ni kifafa cha mimba.
Tazama pia: Maji kujaa ghafla kwenye mapafu (acute pulmonary oedema)
Imeandikwa:
29 Oktoba 2026, 16:34:25

