top of page

Mwandishi:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

3 Novemba 2026, 15:48:56

Mabusha (hydrocele)

Mabusha (hydrocele)

Majina mengine: haidrosili; hydrocele (Kiingereza)


Aina ya neno: hali ya ugonjwa


Maana: mkusanyiko wa maji ndani ya tunica vaginalis.


Maelezo zaidi


  • Mara nyingi haina maumivu; uvimbe huwa laini na mwanga wa tochi hupenya (transillumination).

  • Tanzania, ugonjwa wa matende (lymphatic filariasis) ni chanzo kikubwa kwa watu wazima.

  • Mabusha makubwa au yanayoleta usumbufu hutibiwa kwa upasuaji.


Lini umwone mtaalamu wa afya


  • Uvimbe wenye maumivu, mgumu, unaokua haraka, au kwa mtoto zaidi ya mwaka 1–2.

Imeandikwa:

29 Oktoba 2026, 16:34:25

bottom of page