top of page

Mwandishi:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

3 Novemba 2026, 15:48:56

Mafuta yaliyoshiba (saturated fat)

Mafuta yaliyoshiba (saturated fat)

Majina mengine: mafuta shamiri; mafuta yaliyojaa; saturated fat (Kiingereza)


Aina ya neno: neno la lishe


Maana: mafuta ambayo tindikali zake za mafuta hazina viungo viwili (double bonds) kati ya atomi za kaboni, hivyo 'zimeshiba' hidrojeni.


Maelezo zaidi


  • WHO inashauri mafuta yaliyoshiba yasizidi asilimia 10 ya nishati yote ya chakula kwa siku.

  • Badilisha kwa mafuta yasiyoshiba: mafuta ya alizeti, karanga, ufuta, soya, samaki, parachichi.

  • Mafuta ya trans (yanayotengenezwa viwandani kwenye majarini ngumu, vyakula vya kukaanga mara nyingi na vitafunwa vya viwandani) ni hatari zaidi – yaepukwe kabisa.


Tazama pia: Mafuta yasiyoshiba (unsaturated fat), Kiwango cha juu cha lehemu nyepesi (LDL) kwenye damu

Imeandikwa:

29 Oktoba 2026, 16:34:25

bottom of page