top of page
Mwandishi:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
8 Novemba 2026, 11:56:45

Maumivu ya maungio (athralijia)
Majina mengine: athraljia; maumivu ya viungo; arthralgia (Kiingereza); maumivu ya viungo vingi = poliathralijia
Aina ya neno: dalili
Maana: maumivu yanayohisiwa kwenye maungio.
Maelezo zaidi
Visababishi: maambukizi ya virusi (mf. chikungunya, dengue, mafua), majeraha, kuchakaa kwa maungio, gauti, magonjwa ya kinga kushambulia mwili, baadhi ya dawa.
Tofauti na arthritis: athralijia ni maumivu tu; arthritis ni uvimbekinga halisi wa maungio.
Lini umwone mtaalamu wa afya
Maungio kuvimba, kuwa ya moto au mekundu, homa, kushindwa kutembea, au maumivu yanayodumu zaidi ya wiki 6.
Imeandikwa:
29 Oktoba 2026, 16:34:25
bottom of page

