top of page
Mwandishi:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
15 Novemba 2026, 07:51:30
Maumivu ya sikio (otalijia)
Majina mengine: otalgia, earache (Kiingereza)
Aina ya neno: dalili
Maana: maumivu ya sikio.
Maelezo zaidi
Kutoka sikioni: maambukizi ya sikio la kati, uvimbekinga wa mfereji wa nje, nta iliyoziba, kitu kigeni.
Kutoka mbali (referred): meno mabovu, uvimbekinga wa mafindofindo, kiungo cha taya, na kwa watu wazima wavutaji sigara – saratani ya koo.
Usiweke mafuta au dawa za kienyeji sikioni.
Lini umwone mtaalamu wa afya
Homa kali, uvimbekinga nyuma ya sikio, usaha, kizunguzungu, uso kupinda, au maumivu ya kudumu kwa mtu mzima.
Tazama pia: Uvimbekinga wa mfereji wa nje wa sikio (otitis externa), Kutokwa na majimaji sikioni (otorrhoea)
Imeandikwa:
29 Oktoba 2026, 17:28:03
bottom of page

