top of page

Mwandishi:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

8 Novemba 2026, 11:56:45

Mawe ya nyongo (gallstones)

Mawe ya nyongo (gallstones)

Majina mengine: cholelithiasis, gallstones (Kiingereza)


Aina ya neno: ugonjwa


Maana: mawe ndani ya kifuko au mirija ya nyongo.


Maelezo zaidi


  • Vihatarishi: wanawake, unene, ujauzito, umri zaidi ya miaka 40, kupungua uzito haraka, selimundu (mawe ya rangi).

  • Matatizo: uvimbekinga wa kifuko cha nyongo, manjano (jiwe kuziba mrija mkuu), uvimbekinga wa kongosho, maambukizi ya mirija (homa, manjano, maumivu – dharura).

  • Hutambuliwa kwa ultrasound; yenye dalili hutibiwa kwa kuondoa kifuko cha nyongo.


Lini umwone mtaalamu wa afya


  • Maumivu ya tumbo la juu kulia yanayodumu zaidi ya masaa machache, homa, manjano au kutapika.


Tazama pia: Maumivu ya mawe ya nyongo (biliary colic), Kifuko cha nyongo (gallbladder)

Imeandikwa:

29 Oktoba 2026, 17:28:03

bottom of page