top of page

Mwandishi:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

29 Oktoba 2026, 17:11:16

Mboni zisizo sawa (anisokoria)

Mboni zisizo sawa (anisokoria)

Majina mengine: anisokoria; anisocoria (Kiingereza)


Aina ya neno: kiashiria


Maana: tofauti ya kipenyo cha mboni (pupil) kati ya jicho la kulia na la kushoto.


Maelezo zaidi


  • Tofauti ya chini ya mm 1 isiyobadilika kwa mwanga mara nyingi ni ya kawaida.

  • Visababishi vya ugonjwa: jeraha la kichwa, shinikizo ndani ya fuvu, kiharusi, kuvimba kwa jicho, matone ya dawa ya macho, Horner's syndrome.

  • Mtaalamu hupima mwitikio wa mboni zote mbili kwa mwanga na giza.


Lini umwone mtaalamu wa afya


  • Mboni kutofautiana ghafla, hasa baada ya jeraha la kichwa, au pamoja na maumivu ya kichwa, kope kulegea, kuona vitu viwili au kusinzia – ni dharura.

Imeandikwa:

29 Oktoba 2026, 16:34:25

bottom of page