top of page
Mwandishi:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
29 Oktoba 2026, 17:11:16
Mikazo ya Braxton Hicks
Majina mengine: mikazo ya Braxton; uchungu bandia; Braxton Hicks contractions (Kiingereza)
Aina ya neno: neno la ujauzito
Maana: mikazo ya mazoezi ya mfuko wa uzazi.
Maelezo zaidi
Huhisiwa zaidi kuanzia miezi mitatu ya mwisho ya ujauzito.
Tofauti na uchungu halisi: haijaongezeka nguvu wala kukaribiana, hupungua ukipumzika, ukibadilisha mkao au ukinywa maji.
Uchungu halisi huja kwa mpangilio, huongezeka nguvu na kukaribiana.
Lini umwone mtaalamu wa afya
Mikazo ikija kwa mpangilio (kila dakika 5 au chini), ikiambatana na maji kutoka, damu, au kabla ya wiki 37 – nenda kituo cha huduma za afya.
Tazama pia: Awamu hai ya uchungu wa kuzaa (active phase of labour)
Imeandikwa:
29 Oktoba 2026, 16:34:25
bottom of page

