Mwandishi:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
29 Oktoba 2026, 17:11:16
Mkanda wa jeshi (herpes zoster)
Majina mengine: hepaz zosta; shingles, herpes zoster (Kiingereza)
Aina ya neno: ugonjwa
Maana: kuamka tena kwa kirusi varicella-zoster kwenye neva moja.
Maelezo zaidi
Dalili: maumivu, kuwasha au kuungua kwenye eneo moja, kisha upele na malengelenge kwa mstari (mara nyingi kifua, mgongo au uso).
Kwenye uso: huweza kuathiri jicho, au sikio (vetigo, kupooza kwa uso – Ramsay Hunt).
Mkanda wa jeshi kwa kijana unaweza kuashiria VVU – pima.
Dawa (acyclovir) huanzwa mapema ndani ya siku 3; maumivu yanaweza kubaki baada ya kupona (postherpetic neuralgia).
Lini umwone mtaalamu wa afya
Upele karibu na jicho, kwenye uso, kwa mwenye kinga dhaifu, au maumivu makali – mwone mtaalamu mapema.
Tazama pia: Malengelenge ya sehemu za siri (genital herpes)
Imeandikwa:
29 Oktoba 2026, 16:34:25

