Mwandishi:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
3 Novemba 2026, 15:48:56

Sukari kupanda (hyperglycaemia)
Majina mengine: damusuziada; haipaglaisimia; hyperglycaemia (Kiingereza)
Aina ya neno: hali ya ugonjwa
Maana: glukosi ya damu kuwa juu kuliko kiwango cha kawaida.
Maelezo zaidi
Dalili: kiu kupita kiasi (polidipsia), kukojoa mkojo mwingi (poliyuria), uchovu, kuona ukungu, kupungua uzito, vidonda kuchelewa kupona.
Visababishi: kisukari kisichodhibitiwa, kuacha dawa, maambukizi, steroid, msongo.
Sukari ya juu sana inaweza kuleta hali za dharura (DKA au HHS): kutapika, kupumua kwa kina na haraka, kuchanganyikiwa.
Lini umwone mtaalamu wa afya
Kutapika, maumivu ya tumbo, kupumua kwa kina, kuchanganyikiwa au kusinzia kwa mwenye sukari ya juu – ni dharura.
Tazama pia: Sukari kushuka (hypoglycaemia); Kisukari (diabetes mellitus)
Imeandikwa:
29 Oktoba 2026, 16:34:25

