top of page

Mwandishi:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

29 Oktoba 2026, 17:28:16

Tegu (tapeworm)

Tegu (tapeworm)

Majina mengine: tapeworm, taeniasis (Kiingereza)


Aina ya neno: ugonjwa (minyoo)


Maana: maambukizi ya minyoo ya Taenia.


Maelezo zaidi


  • Mara nyingi hakuna dalili; wengine huona vipande vyeupe vya minyoo kwenye kinyesi, maumivu ya tumbo au kupungua uzito.

  • Cysticercosis ya ubongo (kutoka kwa mayai ya tegu ya nguruwe) ni chanzo kikubwa cha kifafa katika maeneo yanayofuga nguruwe Tanzania.

  • Hutibiwa kwa dawa (mf. praziquantel au albendazole) kwa ushauri wa mtaalamu.

  • Kinga: kupika nyama vizuri, kunawa mikono, vyoo bora, kufuga nguruwe ndani ya banda.


Lini umwone mtaalamu wa afya


  • Degedege la kwanza kwa mtu mzima, au kuona vipande vya minyoo kwenye kinyesi.


Tazama pia: Degedege (seizure), Minyoo safura (hookworm)

Imeandikwa:

29 Oktoba 2026, 17:28:03

bottom of page