Mwandishi:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
29 Oktoba 2026, 17:11:16
Upungufu wa homoni za pituitari baada ya kujifungua (Sheehan's syndrome)
Majina mengine: sindromu ya Sheehan; Sheehan's syndrome, postpartum pituitary necrosis (Kiingereza)
Aina ya neno: ugonjwa (wa homoni)
Maana: kufa kwa tishu za pituitari kwa kukosa damu baada ya kuvuja damu kwingi kwa uzazi.
Maelezo zaidi
Dalili: maziwa kutotoka, hedhi kutorudi, kupotea kwa nywele za kwapa na sehemu za siri, uchovu, baridi, uzito kuongezeka, sukari na shinikizo la damu kushuka.
Dalili huweza kuja haraka au miaka kadhaa baadaye.
Hutambuliwa kwa vipimo vya homoni; hutibiwa kwa kuchukua homoni zilizopungua maisha yote (mf. haidrokotisoni, homoni ya tezi ya shingo).
Kinga: kuzuia na kutibu haraka kuvuja damu baada ya kujifungua (PPH) – kujifungulia kituo cha afya.
Lini umwone mtaalamu wa afya
Baada ya kujifungua na kuvuja damu nyingi: kushindwa kunyonyesha, uchovu mkubwa, kizunguzungu au hedhi kutorudi.
Tazama pia: Tezi ya pituitari (pituitary gland), Upungufu wa homoni za tezi ya adrenal (adrenal insufficiency)
Imeandikwa:
29 Oktoba 2026, 16:34:25

