top of page
Mwandishi:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
29 Oktoba 2026, 17:11:16
Upungufu wa homoni za tezi ya shingo (hypothyroidism)
Majina mengine: upungufu wa homoni thairoidi; upungufu wa homoni tezi shingo; hypothyroidism (Kiingereza)
Aina ya neno: ugonjwa wa homoni
Maana: upungufu wa homoni T4 na T3.
Maelezo zaidi
Visababishi: kinga kushambulia tezi (Hashimoto), upungufu wa madini joto (iodine), baada ya upasuaji au iodine ya mionzi, baadhi ya dawa.
Dalili: uchovu, kuongezeka uzito, kuhisi baridi, ngozi kavu, nywele kunyonyoka, kufunga choo, hedhi nzito, sonona, mapigo ya moyo kwenda polepole, tezi kuvimba (goita).
Kwa watoto wachanga huleta udumavu wa akili na mwili usipotibiwa mapema.
Hutibiwa kwa vidonge vya levothyroxine kila siku; chumvi yenye madini joto huzuia upungufu wa iodine.
Tazama pia: Homoni (hormone)
Imeandikwa:
29 Oktoba 2026, 16:34:25
bottom of page

