top of page
Mwandishi:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
29 Oktoba 2026, 17:11:16
Uvimbe wa neva ya kusikia (acoustic neuroma)
Majina mengine: nyuroma ya akustiki; vestibular schwannoma, acoustic neuroma (Kiingereza)
Aina ya neno: ugonjwa (uvimbe)
Maana: uvimbe wa seli zinazozunguka neva ya kusikia na ya uwiano (vestibulocochlear nerve).
Maelezo zaidi
Dalili: kusikia kunapungua taratibu upande mmoja, mlio masikioni (tinnitus), kizunguzungu au kukosa uwiano; uvimbe ukikua sana, ganzi ya uso au maumivu ya kichwa.
Hutambuliwa kwa kipimo cha kusikia na MRI.
Matibabu: kufuatilia (uvimbe mdogo), mionzi au upasuaji.
Lini umwone mtaalamu wa afya
Kusikia kunapungua upande mmoja tu, hasa pamoja na mlio sikioni au kizunguzungu.
Imeandikwa:
29 Oktoba 2026, 16:34:25
bottom of page

