top of page
Mwandishi:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
8 Novemba 2026, 11:56:45

Uvimbekinga mkali wa ini (acute hepatitis)
Majina mengine: homa ya ini ya ghafla; hepataitis kali; acute hepatitis (Kiingereza); Uvimbe mkali wa ini
Aina ya neno: ugonjwa
Maana: uvimbekinga wa ghafla wa ini unaodumu chini ya miezi 6.
Maelezo zaidi
Visababishi: virusi vya homa ya ini A, B, C, D, E; baadhi ya dawa (mf. dozi kubwa ya paracetamol, dawa za kifua kikuu); pombe; sumu.
Dalili: uchovu, kichefuchefu, kukosa hamu ya kula, maumivu chini ya mbavu za kulia, manjano, mkojo mweusi na kinyesi cha rangi hafifu.
Wengi hupona; wachache hupata ini kushindwa kufanya kazi ghafla au ugonjwa sugu wa ini.
Chanjo huzuia homa ya ini B (na A).
Lini umwone mtaalamu wa afya
Manjano, kuchanganyikiwa, kusinzia sana, kutokwa na damu au kutapika mara kwa mara.
Imeandikwa:
29 Oktoba 2026, 16:34:25
bottom of page

