top of page

Mwandishi:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

8 Novemba 2026, 11:56:45

Uvimbekinga wa utando wa ndani wa moyo (endocarditis)

Uvimbekinga wa utando wa ndani wa moyo (endocarditis)

Majina mengine: endokadaitisi; infective endocarditis (Kiingereza); Uvimbe wa utando wa ndani wa moyo


Aina ya neno: ugonjwa


Maana: maambukizi ya endocardium, hasa valvu za moyo.


Maelezo zaidi


  • Walio hatarini: wenye ugonjwa wa valvu (mf. kutokana na homa ya baridi yabisi), valvu bandia, ugonjwa wa moyo wa kuzaliwa, wanaojidunga dawa za kulevya.

  • Dalili: homa ya muda mrefu, uchovu, kupungua uzito, mvumo mpya wa moyo, madoa ya damu chini ya kucha, vidole rungu.

  • Hutambuliwa kwa kuotesha damu mara kadhaa na echocardiogram; hutibiwa hospitali kwa antibiotiki za mshipa wiki 4–6 (STG 2026).

  • Usafi wa meno ni muhimu kwa wenye ugonjwa wa valvu.


Lini umwone mtaalamu wa afya


  • Homa isiyoisha kwa mtu mwenye ugonjwa wa moyo au valvu bandia.


Tazama pia: Bakteria kwenye damu (bakteremia)

Imeandikwa:

29 Oktoba 2026, 16:34:25

bottom of page