top of page

Mwandishi:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

8 Novemba 2026, 11:56:45

Uvimbekinga wa utando wa tumbo (peritonaitisi)

Uvimbekinga wa utando wa tumbo (peritonaitisi)

Majina mengine: peritonaitisi; peritonitis (Kiingereza); Uvimbe wa utando wa tumbo


Aina ya neno: ugonjwa / dharura


Maana: uvimbekinga wa peritoniamu.


Maelezo zaidi


  • Visababishi: kidole tumbo kupasuka, kidonda cha tumbo kutoboka, utumbo kutoboka (mf. homa ya matumbo), majeraha ya tumbo, maambukizi ya via vya uzazi, baada ya upasuaji au kutoa mimba kusiko salama; kwa wenye maji tumboni (ini kusinyaa) au wanaosafishwa damu kupitia tumbo, huweza kutokea bila kutoboka.

  • Dalili: maumivu makali ya tumbo yanayoongezeka ukijongea au kukohoa, tumbo kukakamaa, homa, kutapika, tumbo kujaa gesi, kushindwa kutoa haja.

  • Hutibiwa kwa antibiotiki kwenye mshipa, maji, na mara nyingi upasuaji wa kurekebisha chanzo.


Lini umwone mtaalamu wa afya


  • Maumivu makali ya tumbo pamoja na tumbo kukakamaa, homa au kutapika – nenda hospitali mara moja; usile wala kunywa wakati unasubiri.


Tazama pia: Kipimo cha kuotesha majimaji ya peritoniamu, Uvimbe ndani ya tumbo (abdominal mass)

Imeandikwa:

29 Oktoba 2026, 16:34:25

bottom of page