top of page

Mwandishi:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

3 Novemba 2026, 15:48:56

Uwiano wa uzito na urefu (BMI)

Uwiano wa uzito na urefu (BMI)

Majina mengine: BMI; Body Mass Index (Kiingereza); uwiano wa uzito wa mwili


Aina ya neno: kipimo cha afya


Maana: uzito (kilo) ukigawanywa kwa urefu (mita) mara urefu (mita).


Maelezo zaidi


  • Mfano: kilo 70, urefu mita 1.70 → 70 ÷ (1.70 × 1.70) = 24.2.

  • Kwa watu wazima: chini ya 18.5 = uzito pungufu; 18.5–24.9 = kawaida; 25–29.9 = uzito uliozidi; 30 na zaidi = unene uliokithiri.

  • Kwa watoto, BMI hupimwa kwa chati za umri na jinsia.

  • BMI haipimi mafuta moja kwa moja; mzunguko wa kiuno pia ni muhimu.

Imeandikwa:

29 Oktoba 2026, 16:34:25

bottom of page