Mwandishi:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
3 Novemba 2026, 15:48:56

Vipele vya moluskam (molluscum contagiosum)
Majina mengine: vipele moluskam ambukizi; molluscum contagiosum (Kiingereza)
Aina ya neno: ugonjwa wa ngozi
Maana: maambukizi ya virusi vya pox (molluscum contagiosum virus) kwenye tabaka la juu la ngozi.
Maelezo zaidi
Huambukizwa kwa kugusana ngozi kwa ngozi, taulo, nguo, na kujikuna (kusambaa sehemu nyingine za mwili).
Kwa wengi hupotea vyenyewe ndani ya miezi 6–18 bila matibabu; usivikamue.
Vipele vingi, vikubwa au vya usoni kwa mtu mzima huashiria kinga dhaifu – pima VVU.
Matibabu yanapohitajika: kugandisha (cryotherapy), kukwangua, au dawa za kupaka kwa ushauri wa mtaalamu.
Lini umwone mtaalamu wa afya
Vipele vikiwa vingi sana, kwenye macho au kope, vikiwa vyekundu na kuuma (maambukizi), au kwa mtu mzima sehemu za siri.
Tazama pia: Sunzua za sehemu za siri (genital warts), VVU (HIV)
Imeandikwa:
29 Oktoba 2026, 16:34:25

