top of page

Mwandishi:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

29 Oktoba 2026, 17:11:16

Wasiwasi wa jumla (generalised anxiety disorder)

Wasiwasi wa jumla (generalised anxiety disorder)

Majina mengine: GAD; generalised anxiety disorder (Kiingereza)


Aina ya neno: ugonjwa wa afya ya akili


Maana: wasiwasi wa kudumu, usio na sababu maalum na unaoathiri maisha.


Maelezo zaidi


  • Dalili: kuhangaika, uchovu, kushindwa kutulia akili, hasira, misuli kukaza, usingizi mbaya; pia mpapatiko wa moyo, jasho, kizunguzungu.

  • Mara nyingi huambatana na sonona.

  • Msaada: tiba ya kisaikolojia (CBT), mazoezi, mbinu za kupumzisha akili, dawa kwa maelekezo ya mtaalamu; epuka pombe na kafeini nyingi.


Lini umwone mtaalamu wa afya


  • Wasiwasi unapozuia kazi, masomo au mahusiano, au pamoja na mawazo ya kujidhuru.


Tazama pia: Mpapatiko wa moyo (palipitesheni)

Imeandikwa:

29 Oktoba 2026, 16:34:25

bottom of page