top of page

Kamusi Tiba ya ULY CLINIC

Antibody ni nini?

Antibody

Ni protini zinazozalishwa kwenye damu kuitikia uwepo wa antijeni kwenye damu.

Antigen ni nini?

Antigen

Ni molekuli au sehemu ya kemikali inayotambulika na mfumo wa kinga kama kitu kigeni, na kusababisha mwili kutoa kinga (antibodi) dhidi yake.

Antijen

Antijeni

Ni protini yenye uwezo wa kuamsha mfumo wa kinga ya mwili kuzalisha antibodi.

Antioxidant ni nini?

Antioxidant

Kizimua oksijeni huru ni elementi(dutu) inayopunguza au kuzuia madhara yanayotokana na chembe huru za oksijeni, ambazo zinaweza kuharibu seli kupitia mchakato wa oksidesheni. Kizimua oksijeni huru hufanya kazi kwa kutoa elektroni au kuzuia mnyororo wa oksidesheni, hivyo kulinda seli na mifumo ya mwili dhidi ya uharibifu wa kemikali.Dutu hizi hupatikana kiasili mwilini au kupitia vyakula na mimea, kama vile vitamini C, vitamini E, na misombo ya mimea yenye kinga ya kibiolojia.

Antitoxin ni nini?

Antitoxin

Ni kinga (antibodi) inayozalishwa na mwili au kutolewa kutoka nje ambayo husaidia kupambana na sumu (toxins) zinazotolewa na vijidudu hatari kama bakteria.

bottom of page