top of page

Kamusi Tiba ya ULY CLINIC

Aortic aneurism ni nini?

Aortic aneurism

Aortic aneurism ni neno tiba lenye jina la kiswahili la anyurizimu ya Aota. Anyurizimu ya aota ni hali ya kitabibu inayohusisha kupanuka au kudhoofika kwa ukuta wa mshipa mkubwa wa damu unaotoka moyoni (Aota).

Aortic aneurism(rupture) ni nini?

Aortic aneurism(rupture)

Anyurizimu ya aota ya tumbo ni upanuzi usio wa kawaida wa sehemu ya mshipa wa damu wa aota uliopita tumboni unaosababisha kuta zake kupanuka, kushikilia shinikizo, na hatimaye kupasuka. Anyurizimu ya Aota ya tumbo iliyopasuka ni dharura ya kitabibu inayoweza kusababisha kupoteza damu kwa haraka na hatari ya maisha, mara nyingi kutokana na mapungufu wa kolajeni au shinikizo la juu la damu.

Aota mputo

Aota mputo

Aota mputo ni kujaa au kuvimba kwa kuta za aota kiasi cha kutengeneza mwonekano puto lililojaa upepo. Magonjwa ya kuambukiza, kijeni na majeraha yanayodhaifisha kuta za mshipa huu hupelekea dalili hii.

Apathy ni nini kwa kiswahili?

Apathy

Apathi ni hali ya kitabibu inayojitokeza kwa kupungua au kukosekana kwa hisia, hamu, au msukumo wa kushughulika na mazingira ya nje au masuala binafsi. Mtu mwenye apathi huonekana kutokuwa na motisha, kutojali shughuli za kila siku, au kukosa mwitikio wa kihisia kwa matukio yanayomzunguka.

Aphasic agraphia ni nini kwa kiswahili?

Aphasic agraphia

Aphasic Agraphia hufahamika kwa kiswahili kama Agrafia ya afezia ambapo ni aina ya agrafia (kupoteza au kuharibika kwa uwezo wa kuandika) inayotokea pale ambapo mtu ana afezia, yaani tatizo la lugha linalosababishwa na uharibifu katika maeneo ya ubongo yanayohusika na uzalishaji na uelewa wa lugha.

bottom of page