top of page

Kamusi Tiba ya ULY CLINIC

Kipimo cha kuotesha tishu ni nini?

Kipimo cha kuotesha tishu

Pia huitwa kipimo cha kuotesha vimelea kutoka kwenye tishu, ni kipimo cha maabara kinachotumika kutambua bakteria, fangasi au vimelea wengine wanaoweza kusababisha maambukizi kwenye tishu za mwili. Sampuli ya tishu huchukuliwa kutoka kwenye eneo linaloshukiwa kuwa na maambukizi, kwa mfano wakati wa upasuaji, kutoka kwenye jeraha, jipu au tishu iliyoathirika, kisha hupelekwa maabara kwa ajili ya kuotesha na kutambua vimelea

Kipimo cha kuotesha majimaji ya perikadiamu ni nini?

Kipimo cha kuotesha majimaji ya perikadiamu

pia huitwa kipimo cha kuotesha vimelea kwenye majimaji ya perikadiamu, ni kipimo cha maabara kinachotumika kutambua bakteria au vimelea wengine wanaoweza kusababisha maambukizi kwenye mfuko unaozunguka moyo (perikadiamu). Sampuli ya majimaji ya perikadiamu huchukuliwa kwa utaratibu unaoitwa perikadiosentesisi, kisha hupelekwa maabara kwa ajili ya kuotesha na kutambua vimelea.

Kipimo cha kuotesha majimaji ya pleura ni nini?

Kipimo cha kuotesha majimaji ya pleura

Kipimo cha kuotesha majimaji ya pleura

Kipimo cha kuotesha majimaji ya peritoniamu ni nini?

Kipimo cha kuotesha majimaji ya peritoniamu

Pia huitwa kipimo cha kuotesha vimelea kwenye majimaji ya peitoniamu, ni kipimo cha maabara kinachotumika kutambua bakteria au vimelea wengine wanaoweza kusababisha maambukizi ndani ya tundu la tumbo. Sampuli ya majimaji ya peitoniamu huchukuliwa kwa utaratibu unaoitwa parasentesisi, hasa kwa mtu mwenye majimaji mengi tumboni (ascites) au anayeshukiwa kuwa na maambukizi ndani ya tundu la tumbo.

Kipimo cha kuotesha majimaji ya maungio ni nini?

Kipimo cha kuotesha majimaji ya maungio

Pia huitwa kipimo cha kuotesha vimelea kwenye majimaji ya maungio, ni kipimo cha maabara kinachotumika kutambua bakteria au vimelea wengine wanaoweza kusababisha maambukizi kwenye maungio. Sampuli ya majimaji ya maungio ya mwili huchukuliwa kwa kutumia sindano kupitia utaratibu unaoitwa arthrosentesisi, kisha hupelekwa maabara kwa ajili ya kuotesha na kutambua vimelea.

bottom of page