top of page

Kamusi Tiba ya ULY CLINIC

Balanitis

Balanitis

Balanitis ni neno tiba lenye jina la Kiswahili la Balanaitisi ambapo ni hali ya kitabibu inayohusisha uvimbe au uchochezi wa kichwa cha uume. Hali hii huathiri wanaume au wavulana, hasa wale wasiotahiriwa, na inaweza kusababishwa na maambukizi, mzio, usafi duni, au magonjwa mengine ya msingi.

Ballance’s sign

Ballance’s sign

Ballance’s sign ni neno tiba lenye jina la Kiswahili la Ishara ya Ballance ambaypo ni dalili ya kitabibu inayopatikana katika majeraha ya wengu (Bandama), hasa pale kunapokuwa na kuvuja damu ndani ya tumbo (hemoperitoniamu). Dalili hii hudhihirika kwa kupatikana kwa ugumu usiobadilika upande wa kushoto wa tumbo kutokana na damu iliyoganda karibu na wengu, huku upande wa kulia wa tumbo ukionyesha ulaini unaobadilika kutokana na damu iliyo huru inayosogea kulingana na mkao wa mgonjwa.

Ballet’s sign

Ballet’s sign

Ballet’s sign ni neno tiba lenye jina la Kiswahili la Ishara ya Ishara ya Ballet ambayo ni dalili ya kitabibu inayojitokeza pale ambapo misuli ya nje ya macho inayohusika na mjongeo wa macho hupooza au kudhoofika, hivyo mgonjwa hushindwa kusogeza macho juu, chini au pembeni kwa hiari licha ya mgonjwa kuwa na mjongeo wa hiari kwenye mwitikio wa mwanga katika mboni. Ishara hii ni kiashiria cha usumu wa thairoid.

Barlow’s sign

Barlow’s sign

Barlow’s sign ni nini kwa kiswahili?

Barré’s pyramidal sign

Barré’s pyramidal sign

Ni neno tiba lenye jina la Kiswahili la Ishara ya Barré ya njia ya piramidi ambapo ni kipimo cha kitabibu kinachotumiwa kutambua udhaifu wa mfumo wa neva wa juu unaotokana na uharibifu wa njia ya piramidi (njia ya kotikospaino ).

bottom of page