top of page

Kamusi Tiba ya ULY CLINIC

Kichomi

Kichomi

Ni maumivu makali na ya ghafla yanayoweza kuwa ya kuchomwa mshale au kisu au kama kukatwa na kitu kikali.

Kidney stone

Kidney stone ni nini?

Kidole Rungu ni nini?

Kidole Rungu

Ni hali ambapo ncha za vidole huongezeka ukubwa na kuwa pana na za mviringo, huku kucha zikiwa zimejikunja zaidi na kuwa na mwonekano wa mviringo. Si ugonjwa wenyewe bali ni ishara inayoweza kuhusishwa na magonjwa mbalimbali, hasa magonjwa sugu ya mapafu kama saratani ya mapafu, maambukizi sugu ya mapafu na baadhi ya magonjwa ya tishu za mapafu.

Kimeng'enya

Kimeg'enya

Kimeng’enya ni kichocheo cha kibaolojia kinachoongeza kasi ya mwitikio wa ki bayokemia bila mabadiliko yoyote.

Kinena ni nini?

Kinena

Ni eneo la mwili lililopo chini ya tumbo na mbele ya sehemu za siri, juu ya mfupa wa kinena. Kwa mwanamke, eneo hili liko mbele ya vulva na linahusisha sehemu inayojulikana kama eneo la kinena la mbele.

bottom of page