top of page

Kamusi Tiba ya ULY CLINIC

Agrafia ya Nafasi ni nini?

Agrafia ya Nafasi

Agrafia ya nafasi hufahamika kwa lugha nyingine kama Spatial Agraphia, ni aina ya agrafia inayotokea pale ambapo mtu hushindwa kuandika kwa mpangilio sahihi kutokana na kuharibika kwa uwezo wa kutambua na kupanga nafasi. Katika hali hii, mtu anaweza kuwa na uelewa mzuri wa lugha na uwezo wa kuunda maneno sahihi, lakini hushindwa kuyaweka vizuri kwenye maandishi kwa sababu mfumo wa utambuzi wa nafasi umeathirika.

Agrafia ya Tahajia ni nini?

Agrafia ya Tahajia

Agrafia ya tahajia ni aina ya agrafia inayojitokeza pale ambapo mtu hushindwa kuandika maneno kwa tahajia sahihi licha ya kuwa na uwezo wa kushika kalamu na kupanga sentensi. Katika hali hii, tatizo liko kwenye mifumo ya ubongo inayohusika na kumbukumbu ya maneno, sauti za lugha, na uhusiano kati ya sauti na maandishi, na si kwenye nguvu ya misuli au uelewa wa jumla wa lugha.

Agraphia ni nini kwa kiswahili?

Agraphia

Ni upungufu wa uwezo wa kuandika kwa mtu ambaye ana akili na uwezo wa kuona na kusikia kawaida. Hali hii husababishwa na uharibifu wa sehemu za ubongo zinazohusika na uandishi.

Akalazia (Achalasia) ni nini?

Akalazia (Achalasia)

Akalazia ni ugonjwa unaofanya chakula na vinywaji vipite kwa shida kutoka kwenye umio kwenda tumboni kutokana na misuli ya umio na valve ya chini ya umio kushindwa kufanya kazi ipasavyo. Ugonjwa huu unaweza kutibiwa kwa njia mbalimbali ikiwa utagunduliwa mapema.

Allis’ sign ni nini kwa kiswahili?

Allis’ sign

Ni ishara inayotumika kutambua kutofanana kwa urefu wa miguu kwa mtoto, inayojulikana pale kidole cha mguu mmoja unapokuwa juu kuliko kingine wakati mtoto ameketi na magoti yameangaliwa.

bottom of page