top of page

Kamusi Tiba ya ULY CLINIC

Maumivu kwenye nyonga ni nini?

Maumivu kwenye nyonga

Ni hali ambapo mtu hupata maumivu yanayotokea ndani ya eneo la nyonga, yaani sehemu yenye viungo mbalimbali vya ndani kama mfuko wa uzazi, ovari, mirija ya uzazi, kibofu cha mkojo, utumbo na tezi dume kwa wanaume. Aina hii ya maumivu mara nyingi haihusiani moja kwa moja na mifupa ya nyonga, bali hutokana na matatizo ya viungo vilivyomo ndani ya eneo hilo.

Maumivu wakati wa kumeza (Odinofagia) ni nini?

Maumivu wakati wa kumeza

Maumivu wakati wa kumeza (odinofagia) ni dalili inayoonyesha kuwepo kwa tatizo kwenye koo au umio. Kutafuta chanzo mapema ni muhimu hasa ikiwa dalili zinaendelea au zinaambatana na kupungua uzito.

Maumivu ya nyonga ni nini?

Maumivu ya nyonga

Ni hali ambapo mtu hupata maumivu yanayotokana na muundo wa nyonga wenyewe (pevisi), ambao unajumuisha mifupa ya nyonga, viungo vinavyounganisha mifupa hiyo, misuli, tendoni, mishipa ya fahamu na tishu zinazozunguka eneo la nyonga. Maumivu haya mara nyingi huhusiana na mfumo wa mifupa na misuli ya nyonga, badala ya viungo vilivyopo ndani ya eneo la nyonga.

Michomo ya kinga ya mwili

Mchomokinga

Ni tendo asili la mwili kuitika kwenye vichokoza mwili vya hatari kama vile bakteria, virusi, chembe zenye jeraha au vikereketa mwili kwa kuzalisha chembe zinazopelea kuondoa vichokozi au ugonjwa.

Mesenteric artery ischaemia

Mesenteric artery ischaemia

Mesenteric artery ischaemia ni nini kwa kiswahili?

bottom of page