top of page

Kamusi Tiba ya ULY CLINIC

Amnesia ni nini?

Amnesia

Ni upungufu wa uwezo wa kukumbuka taarifa au matukio ya zamani, mara nyingi kutokana na kuumia au ugonjwa wa ubongo. Inaweza kuwa ya muda mfupi au ya kudumu kulingana na chanzo chake.

Amniotic fluid ni nini?

Amniotic fluid

Ni maji yanayozunguka mtoto tumboni ndani ya mfuko wa amnioni, ambayo humlinda mtoto, kumsaidia kuendeleza viungo, na kuwezesha harakati za mtoto wakati wa mimba.

Amnizia ni nini?

Amnizia

Ni upungufu wa uwezo wa kukumbuka taarifa au matukio ya zamani, mara nyingi kutokana na kuumia au ugonjwa wa ubongo. Inaweza kuwa ya muda mfupi au ya kudumu kulingana na chanzo chake.

Amnizia ya histeriko

Amnizia ya histeriko

Ni upotevu wa kumbukumbu zote unaoanza ghafla na kudumu kwa muda mrefu na hujitofautisha kwa kuambatana na ukanganyifu na huwa na mahusiano ya kisaikolojia.

Amnizia ya kweli

Amnizia ya kweli

Ni upotevu wa kumbukumbu unaotokana na madhaifu ya ufanyaji kazi wa ubongo wa temporo, sifa mojawapo ya amnizia hii ni kubaki na mabaki ya kumbukumbu

bottom of page