top of page

Imeandikwa na daktari wa ulyclinic

​

​

Sindrome ya kinywa kuwaka moto

 

Sindromu ya kinywa kuwaka modo ni tatizo lisilojulikana kisababishi chake, tatizo hili huleta dalili endelevu za kuhisi unaungua ndani yakinywa(mdomo), haswa, ikihusisha ulimi na maumivu hayo yanaweza kusambaa kwenye midomo na maeneo mengine ya ndani ya kinywa.

​

Sindromu halisi ya kinywa kuwaka moto huambatana na dalili za kubadilika kwa ladha ya chakula na hisia za kinywa kukauka.

 

Dalili hii hutokea sana kwa wamama wanaoelekea kwenye miaka ya koma hedhi au walio kwenye koma hedhi, ingawa inaweza kutokea kwenye kipindi cha umri wowote ule.

 

Ili mtu asemekane ana tatizo la sindromu ya kinywa kuwaka moto, vipimo vyote na sababu zinazofahamika kusababisha kinywa kuwaka moto lazima ziwe zimepimwa na kupata jibu la kuwa hakuna tatizo ndani ya mwili isipokuwa dalili hiyo tu.

​

Kuna makundi tofauti ya sindromu ya kinywa kuwaka moto kutokana na dalili yaani

 

Aina ya kwanza

Mgonjwa anakuwa hana dalili aamkapo asubuh,  dalili ziaanza kuonekana baada ya kuamka tu na huendelea kuongezeka siku nzima. Dalili za usiku huwa za namna ya tofauti. Dalili hii huweza kuonekana pia kwa wagonjwa wenye kisukari na upungufu wa viinirishi mwilini

​

​

 

Soma zaidi kuhusu aina na  dalili na matibabu kwa kubonyeza hapa au Soma mada ingine ya kuhusu Ulimi kuwaka moto hapa,

 

Endapo umepatwa na dalili hizi wasiliana na daktari wako ili kupata vipimo na uchunguzi pamoja na tiba

​

​

Kuomba tiba kutoka kwa madaktari wa ulyclinic bonyeza hapa, au piga namba za simu chini ya tovuti hii kukutana na daktari

 

Imeboreshwa 9.03.2020

 

​

Utangulizi
Aina
bottom of page