top of page
Mobile clinic in Tanzania- ulyclinic

Tafsiri kwenda kiingeleza

​

Huduma za afya zinazotembea na Huduma Tiba nyumbani Tanzania

 

 

ULY clinic imeanza kutoa huduma za afya zinazomfuata mteja karibu na sehemu anayoishi na huduma za nyumbani

 

Huduma hizi zinazotembea kwa sasa zinapatikana Jijini Arusha na wilaya zake.

​

Timu ya ULY CLINIC imejipanga kukupatia huduma zenye ubora wa juu zinazojali muda wako. Tunajali muda wako kwa sababu muda ni mali

​

​

Je unaishi Arusha?

​

Endapo upo jijini Arusha huduma za afya na ULY CLINIC zitakufikia  karibu na wewe, baadhi ya huduma unazoweza pata  ni;

​

  • Kuandikiwa  na kuletewa dawa

  • Huduma za kuchomwa dozi yako ya sindano

  • Huduma za kuonana na daktari ikiwa pamoja na kuonana na daktari wa  kawaida na daktari wabobezi kwenye fani mbalimbali.

  • Checkup ya mwili

  • Huduma ya kwanza

  • Huduma ya Kutunza kidonda

  • Huduma ya vipimo mbalimbali za vipimo vya maabara

  • Huduma za uzazi wa mpango na kujifungua

  • Kuongezewa dawa kwa wale wanaotumia dawa muda mrefu(Wagonjwa wa kisukari, UKIMWI, Shinikizo la juu la damu n.k)

  • Kufanyiwa upasuaji mdogo ikiwa pamoja na kutahiliwa, kushonwa majeraha, kuondolewa nyuzi n.k)

  • Huduma za chanjo kama chanjo ya Hepatitis B, tetenus n.k

  • Ushauri lishe kwa wagonjwa wa kisukari, presha ya juu na saratani

  • Ushauri namna ya kutumia huduma za application ya ULY CLINIC

  • Na huduma zingine zaidi

​

Je naweza mudu gharama zenu za matibabu?

​​

Ndio. Dhumuni la huduma hizi zinazotembea ni kuwapa wateja huduma kwa gharama ya chini kabisa kulingana na uwezo wa mtu. Hii ndio maana gharama zetu ni za chini ukilinganisha na gharama za hospitali.

​

​

ULY CLINIC inajali afya yako na kuzingatia sera ya usiri wa taarifa zako za afya.

​

Kwa taarifa zaidi na kupata huduma wasiliana nasi kwa namba za simu chini ya tovuti hii au kubonyeza hapa

​

Pakua application yetu kwa kubonyeza hapa.

​

Imeboreshwa mara ya mwisho 28.06.2020

bottom of page