Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Benjamin L, MD
4 Juni 2025, 06:10:25

Komahedhi
Koma hedhi ni hali ya kawaida ya kibaolojia ambapo mwanamke hukoma kupata hedhi kwa kipindi kisichopungua miezi 12 mfululizo bila uwepo wa ujauzito au ugonjwa mwingine unaoathiri mzunguko wa hedhi. Kwa kawaida, hutokea kati ya umri wa miaka 45 hadi 55, na wastani wa miaka ya kuingia ni miaka 50–51.
Ikiwa koma hedhi hutokea kabla ya umri wa miaka 40, huitwa koma hedhi ya mapema au kutojitosheleza kwa homoni kutokana na tatizo linaloanzia kwenye ovari, na huhitaji uchunguzi wa kitabibu.
Hatua za kukoma kwa hedhi
Kipindi kabla ya kukoma kwa hedhi- Hutokea kabla ya kufikisha umri wa miaka 40 huambatana na dalili mbalimbali
Kipindi cha kuelekea koma hedhi- Kipindi hiki huambatana na dalili za kufikia mwisho wa hedhi kukoma
Koma hedhi- Hiki ni kipindi cha umri wa miaka 45 hadi 55 wastani wake ni miaka 50
Kipindi baada ya koma hedhi- Hiki ni kipindi baada ya hedhi kukoma na kutuoina angalau kwa miezi 12 mfululizo
Visababishi vya koma hedhi
Visababishi vya kawaida:
Kupungua na hatimaye kusimama kwa uzalishaji wa mayai kutoka ovari.
Upungufu au kukoma kwa homoni za uzazi: estrogen na progesterone.
Koma hedhi ya mapema (kabla ya miaka 40):Sababu nyingi hazijulikani, lakini baadhi ya visababishi maalum ni:
Upasuaji wa kuondoa ovari
Tiba ya saratani (kemotherapi au mionzi)
Magonjwa ya kurithi kama Down syndrome
Magonjwa ya kinga mwilini (mfano: Ugonjwa wa Addison’s)
Dalili za koma hedhi
Kutokwa na jasho usiku
Hali ya joto la ghafla mwilini
Kukosa usingizi
Hali ya huzuni au msongo wa mawazo
Kukosa hamu ya tendo la ndoa
Uke kuwa mkavu na usumbufu wakati wa tendo la ndoa
Kukojoa mara kwa mara au kwa dharura
Ngozi kusinyaa, nywele kupungua
Uzito kuongezeka
Kuongezeka kwa lehemu (cholesterol)
Maumivu ya kichwa
Mifupa kuwa dhaifu (osteoporosis)
Sauti kuwa ndogo au kubadilika
Kukumbwa na uchovu mara kwa mara
Vipimo vya kuchunguza koma hedhi
FSH (follicle stimulating hormone): huongezeka kama ovari zimekoma kazi.
LH (luteinizing hormone): pia huongezeka.
Estrogen (estradiol): kiwango chake hupungua wakati wa koma hedhi.
TSH (thyroid stimulating hormone): hupimwa ili kuondoa uwezekano wa matatizo ya tezi ambayo yanaweza kuathiri mzunguko wa hedhi.
Lipid profile (lehemu): hupima hatari ya magonjwa ya moyo baada ya koma hedhi.
Uzito wa mifupa (DEXA scan): hupima wingi wa madini kwenye mifupa ili kutathmini hatari ya kuvunjika kwa mifupa.
Matibabu
1. Tiba ya homoni mbadala
Dawa zenye estrogen na progesterone hutolewa pamoja ili kupunguza dalili na kulinda mfuko wa uzazi.
Estrogen pekee hutolewa kwa wanawake waliotolewa kizazi.
Angalizo: tiba hii huongeza hatari ya:
Saratani ya matiti na kizazi
Magonjwa ya moyo
Kiharusi
Matatizo ya mishipa ya damu
2. Tiba zisizo za homoni
Vidonge vya vitamini D na kalsiamu
Mazoezi ya kuimarisha mifupa
Chakula chenye protini na madini ya kutosha
Tiba ya kisaikolojia na ushauri nasaha
Kuepuka uvutaji sigara na unywaji pombe
Wakati gani wa kumuona daktari?
Wasiliana na daktari:
Kama una dalili za koma hedhi kabla ya miaka 45
Kama hedhi haipo kwa miezi kadhaa bila sababu ya wazi
Kama dalili za koma hedhi zinaathiri maisha yako ya kila siku
Hitimisho
Koma hedhi ni mabadiliko ya kawaida katika maisha ya mwanamke, lakini yanaweza kuleta changamoto mbalimbali kiafya na kihisia. Uchunguzi wa kitabibu na ushauri wa mapema unaweza kusaidia kudhibiti dalili na kupunguza hatari za kiafya. Elimu kuhusu hatua hizi huwasaidia wanawake kuwa na maisha yenye afya hata baada ya kukoma kwa hedhi.
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Imeandikwa:
6 Mei 2020, 10:25:06
Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini
[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]
Rejea za mada
1. Nelson HD. Menopause. Lancet. 2008 Mar 1;371(9614):760–70.
2. Santoro N, Epperson CN, Mathews SB. Menopausal Symptoms and Their Management. Endocrinol Metab Clin North Am. 2015 Sep;44(3):497–515.
3. Shifren JL, Gass ML. The North American Menopause Society recommendations for clinical care of midlife women. Menopause. 2014 Oct;21(10):1038–62.
4. Avis NE, Crawford SL, Greendale G, Bromberger JT, Everson-Rose SA, Gold EB, et al. Duration of menopausal vasomotor symptoms over the menopause transition. JAMA Intern Med. 2015 Apr;175(4):531–9.
5. Faubion SS, Kuhle CL, Shuster LT, Rocca WA. Long-term health consequences of premature or early menopause and considerations for management. Climacteric. 2015 Aug;18(4):483–91.
6. Soules MR, Sherman S, Parrott E, Rebar R, Santoro N, Utian W, et al. Executive summary: Stages of Reproductive Aging Workshop (STRAW). Climacteric. 2001 Jun;4(4):267–72.
7. Santen RJ, Allred DC, Ardoin SP, Archer DF, Boyd N, Braunstein GD, et al. Postmenopausal hormone therapy: an Endocrine Society scientific statement. J Clin Endocrinol Metab. 2010 Jul;95(7 Suppl 1):s1–66.
8. North American Menopause Society. Management of osteoporosis in postmenopausal women: 2021 position statement. Menopause. 2021 Sep 1;28(9):973–97.
9. Freeman EW, Sammel MD, Lin H, Liu Z, Gracia CR. Duration of menopausal hot flushes: a longitudinal study. Obstet Gynecol. 2011 May;117(5):1095–104.
10. Greendale GA, Lee NP, Arriola ER. The menopause. Lancet. 1999 May 22;353(9152):571–80.
11.Web.Md.Menopause.https://www.webmd.com/menopause/guide/menopause-symptoms-types. Imechukuliwa 10/4/2020
12.Health.Line.Today.Menopause.https://www.healthline.com/health/menopause.Imechukuliwa 10/4/2020
13.Menopause. National Institute on Aging. http://www.nia.nih.gov/health/publication/menopause. Imechukuliwa 10.04.2020
14.Casper RF, et al. Clinical manifestations and diagnosis of menopause. https://www.uptodate.com/home. Imechukuliwa 10.04.2020
15.Longo DL, et al., eds. Menopause and postmenopausal hormone therapy. In: Harrison's Principles of Internal Medicine. 19th ed. New York, N.Y.: McGraw-Hill Education; 2015. http://accessmedicine.mhmedical.com. Imechukuliwa 10.04.2020
16.Nelson LM, et al. Clinical manifestation and evaluation of spontaneous primary ovarian insufficiency (premature ovarian failure). https://www.uptodate.com/home. Imechukuliwa 10.04.2020
17.Menopausal symptoms and complementary health practices. National Center for Complementary and Alternative Medicine. http://nccam.nih.gov/health/menopause/menopausesymptoms. Imechukuliwa 10.04.2020
18.Medical.New.Today.Menopause.https://www.medicalnewstoday.com/articles/155651.Imechukuliwa 10/4/2020
19.Dc Dutta Textbook Gynaecology ISBN 978-93-5152-068-9 written by Hiralal Konar Ukurasa wa 57-60
