Mwandishi: Dkt. Sospeter B, MD, Dkt. Adolf S, MD
Mhariri: Dkt Lugonda B, MD
​
Imeandikwa 10/8/2016
​
Mwasho wa ngozi
Ngozi kuwasha hutokana na mabadiliko ya hisia ya ngozi inayopelekea kujikuna ili kupunguza hali inayohisiwa. Hali hii huleta hisia za kero na mtu kutohisi raha, ngozi kuwasha huweza ambatana au isiambatane na vipele,malengelenge, rangi kubadilika na hali ya ukavu wa ngozi uliyopitiliza.
Hali ya kuwashwa inaweza tokea sehemu Fulani pekee mwilini au mwili mzima. Miwasho ya mda mrefu hutibiwa kwa kugundua na kutbu visababishi kwa kutumia madawa, kuvaa nguo zilizolowekwa maji na matibabu ya mwanga. Matunzo binafsi kama kutumia dawa za kuzuia miwasho na kuoga maji ya baridi huweza kusaidia pia.
Dalili
Unaweza kuwa na ngozi inayowasha sehemu Fulani pekee ya mwili kama kwenye mguu, au kuwashwa mwili wote. Ngozi kuwasha huweza kutokea bila kwua na dalili ambata zozote zile au huweza kuambatana na;
-
Ngozi kuwa nyekundu
-
Mwinuko kwenye ngozi, madoa na malengelenge
-
Magamba kwenye ngozi
Wakati mwingine miwasho hudumu kwa mda mrefu na huweza kuwa miwasho ya hali ya juu, unavyozidi kukwangua eneo linalowasha huendelea kuwasha zaidi na unazidi kukwangua zaidi. Kuvunja mzunguko huu huweza kuwa vigumu, lakini kuendelea kukwangua huweza kujeruhi ngozi na kusababisha maambukizi kutokea.
​
Endelea kusoma kwa kubonyeza kichwa cha mada
​
​
ULY CLINIC inakukumbusha siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya
​
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri zaidi na tiba kwa kubofya linki ya 'Pata tiba au 'Wasiliana nasi' chini ya tovuti hii.
​
Imeboreshwa 30/11/2020