top of page

Imeandikwa na daktari wa ULY-Clinic

Maambukizi wakati wa ujauzito

Je kuwa mjamzito ni kuwa na kinga za mwili za chini?

 

Ujauzito huonyesha hali ya pekee ya kinga ya mwili ya kutoka kwa watu wawili waliotengenezwa kwa jeni ambao hawakataani kwenye upande wa kinga ya mwili. Kinga ya mwili mara nyingi hukataa vitu vigeni vinapoingia kwenye mwili na hili huwa tofauti kwenye ujauzito kwa sababu kinga ya mwili ya mama hushuka ili ujauzito usitambuliwe kwamba ni kitu kigeni. Maambukizi (nimoni, bacteria kwenye figo)wakati wa ujauzito yanaweza kuwa makali zaidi, hii ni kutotokana na udhaifu wa mfumo wa kinga ya mama ila kwa sababu ya mabadiliko ya kianatomia na kifisiolojia katika mwili wa mama mjamzito.

 

Kwanini kuna umuhimu wa kujua maambukizi wakati wa ujauzito?

 

Kujua maambukizi ya wakati wa ujauzito kuna umuhimu kwa sababu mbili. Maambukizi yanaweza kusababisha madhara makubwa na kifo kwa mama na mtoto(kama nimonia ya pneumococcal). Maambukizi haya yanaweza yasimzuru mama lakini yanaweza kumdhuru mtoto si moja kwa moja. Maambukizi mengine yanaweza kuwa hayana umuhimu wa mama lakini hupita kupitia kondo kwenda kwa mtoto na kumdhuru kama maambukizi ya toxoplasma.

Imeboreshwa mara ya mwisho 07.07.2020

ULY Clinic inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchuku hatua yoyote ile inayohusu afya yako.

Wasiliana na daktari wa ULY Clinic kwa elimu zaidi na Tiba kwakubonyeza Pata Tiba au kupiga namba za simu chini ya tovuti hii.

maambukizi wakati wa ujauzito
bottom of page