Utangulizi
Maambukizi yanayoweza kutoa mimba
Magonjwa na maambukizi yanayoweza kusababisha mimba kutoka au kujiffungua kabla ya wakati
​
Imeandikwa na daktari wa ulyclinic
​
Maambukizi ya bakteria ukeni huhusika na kujifungua kabla ya wakati, matibabu ya maambukizi haya kwa wanawake walio kwenye kihatarishi huonekana kusaidia kupunguza ukubwa wa tatizo la kujifungua kabla ya wakati. Maambukizim engine kama yale ya trichomonas, kaswende na Chlamydia yamekuwa yakiambatana na kupasuka kwa chupa ya uzazi kabla ya wakati.
Maambukizi gani huwa yana madhara kwa mama lakini huwa na madhara makubwa kwa mtoto?
Maambukizi ya parvovirus, cytomegalovirus na toxoplasma
​
​
Maambukizi ya parvovirus kwa mjamzito
​
Madhara gani kwa mama na mtoto husababishwa na parvovirus?
Maambukizi ya parvovirus, yakijulikana kama ugonjwa wa tano kwa jina jingine, ni maambukizi yanayotokea kwa lakini sio sana huwa hayaonyeshi dalili au huwa na dalili kiasi tu kwa watu wakubwa. Maambukizi kwa wamama wajawazito hutokea kwa kukutana na watoto walioambukizwa. Hata kama madhara kwa mama huwa hayaonekani na hayana umuhimu, huweza kusababisha madhara kwa kichanga tumboni kwa kuleta upungufu mkali wa damu mtoto kujaa maji na kufa. Utambuzi hutambuliwa vipimo mbalimbali vya damu. Kama maambukizi kwa kichanga tumboni yameonekana na amejaa maji kutokana na kuonekana kwenye kipimo cha ultrasound basi kichanga anaweza kuongezewa damu akiwa tumboni wa mama.
Maambukizi ya Kaswende kwa mjamzito
​
Madhara gani ya kaswende kwa mtoto wakati wa ujauzito?
Maambukizi ya kaswende kwa mtoto huweza kusababisha mlolongo wa matatizo, ikiwepo mtoto maji, kuvimba kwa ini na bandama. Huweza kusababisha pia kujifungua mtoto aliyekufa. Madhara kwa mtoto huweza kuzuiwa kwa kupiwa wamama na kuwapa dawa mwanzoni kabisa mwa ujauzito au kabla ya kupata ujauzito, matibabu hutegemea hatua ya ugonjwa huu wa kaswende. Matibabu hutumia dawa aina ya penicillin na endapo mama ana mzio na dawa hii basi ni lazima apewe dawa ya kuzuia mzio kabla ya kupewa dawa hii.
Ukubwa wa kaswende kwenye jamii umepungua kwenye miaka kumi hii ya hivi karibuni, kutokana na kutambuliwa mapema na kutibiwa. Madhara kwa mtoto ya kuzaliwa yamepungua pia kutokana na sababu iliyotajwa hapo awali.
​
Maambukizi ya VVU kwa mjamzito
​
Maambukizi ya VVU yanadhuru vipi ujauzito?
Kama ilivyo maambukizi yote wakati wa ujauzito, kuna maswala ya mama na mtoto. Kwa mama, suala la msingi ni kudhibiti ugonjwa. Kwa mtoto swala ni kuzuia maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto. Ujauzito hauonekani kusabaisha maambukizi ya VVU kuwa makali.
Dawa za ARV ni salama kipindi cha ujauzito?
Kuna mijadala kuhusu matumizi ya dawa za ARVs kipindi cha ujauzito kama tiba ya VVU. Dawa zinazotumika huwez akuwa sumu, na kuna taarifa kidogo kuhusu usalama wake wakati wa ujauzito. Hata hivyo, usalama wa dawa unatakiwa kulinganishwa na faida anazopata mama na mtoto. Kutegemea ukubwa wa ugonjwa, matibabu dawa huweza kuleta matokeo mazuri y ugonjwa kwa mama. Kwa mtoto, faida huonekana moja kwa moja. Maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto hutegemea mzigo wa virusi ndani ya damu ya mama , matumizi ya dawa za ARVs hupunguza mzigo wa virusi kwenye damu ya mama. Wanawake wajawazito lazima wapewe dawa hata kama ugonjwa hauonekani kama inavyooneshwa na kiwango cha CD4 na mzigo wa virusi. Kwa sasa matibabu ya virusi vya ukimwi wakati wa ujauzito huhusisha matumizi ya muunganiko kutoka kwenye makundi mbalimbali ya ARVs.
Hatua gani zichukuliwe ili kuzuia maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto?
​
Kuzuia maambukizi kwa mama kwenda kwa mtoto tumboni huhusisha hatua nyingi.
-
Kwanza mjamzito mwenye virusi vya ukimwi anatakiwa apate dawa hizi wakati wa mwanzao anapotambulika na VVU.
-
Pili mzigo wa virusi katika damu unazidi kopi 1000 kwa mililita, kujifungua kwa upasuaji kunatakiwa kufanyike haraka.
-
Kitu cha tatu wanawake wenye VVU baada ya kujifungua mtoto anatakiwa kupatiwa dawa za VVU kwa ajili ya kinga kwa kipindi hiki anapokuwa ananyonya maziwa ya mama. Au ainyonye kabisa maziwa endapo hapati dawa hizi.
-
Kujifungua kwa njia ya upasuaji kumeonekana kupunguza maambukizi kwa mtoto kwa wamama wenye mzigo mkubwa wa VVU kwenye damu. Faida ya zake huonekana hata kama chupa ya uzazi imeshapasuka.
Kwa pamoja njia hizo zinaweza kuzuia maambukizi kwa mtoto hadi chini ya asilimia 5. Kama njia zisipochukuliwa na mtoto akazaliwa kwa njia ya kawaida basi mtoto ana asilimia 15-25 kupata maambukizi kutoka kwa mama.
Je wajawazito wanatakiwa kupima mara kwa mara VVU?
Ndio. Wajawazito wanatakiwa kupima maambukizi haya ya VVU kutokana na ratiba iliyowekwak wenye kliniki zao husika. Wajawazito wanatakiwa kupima mwanzo kabisa kabla ya kupata ujauzito na mara mbili au tatu baada ya kupata ujauzito kwa wale tu wenye vihatarishi vya kupata maambukizi haya ya VVU. Upimaji huambatana na ushauri husika kwa mama mjamzito.
​
​
Maambukizi ya rubela kwa mjamzito
​
Nini umuhimu wa kujua maambukizi ya rubella wakati wa ujauzito?
Rubella husababisha sulua, ambao ni ugonjwa usio na shida sana kwa mama, lakini huwezakusababisha shida kubwa kwa mtoto tumboni kwa kudhuru mifumo mbalimbali ikiwa pamoja na mfumo wa fahamu na moyo. Rubella huweza kusababisha kutokuwa kwa mtoto tumboni mwa mama. Maambukizi kwa mtoto hutokea sana endapo mama amepata maambukizi haya mwanzoni kabisa mwa ujauzito. Maambukizi mwanzoni kabisa mwa ujauzito husababisha madhara makubwa kwa kichanga tumboni.
Bahati nzuri, maambukizi kwa mama na madhara kwa mtoto huweza kuzuia kwa chanjo kwa wanawake walio katika umri wa kuzaa. Baadhi ya nchi imeweka kama sheria kwamba kabla ya kuolewa lazima kuwa na cheti kinachoonyesha ushachoma chanjo ya rubella, hata hivyo inamaanisha kabla ya kupata ujauzito ni lazima mwanamke awe ameshachoma sindano hii ya kujikinga na rubella.
​
Maambukizi ya tetekuwanga (varicella ) na herpes zoster kipindi chujauzito.
Maambukizi hayo yote hutasababishwa na kirusi cha varicella zoster. Maambukizi ya awali ya kirusi huyu husababisha madhara kwenye ngozi tu. Maambukizi yakipotea(hujificha katika mishipa ya fahamu) badae huweza kuamshwa tena na vitu mbalimbali kama kushuka kwa kinga ya mwili, maambukizi ya VVU n.k mara hii maambukizi haya husababisha mkanda wa jeshi(kutokea kwenye ukanda unaopitiwa na mshipa wa fahamu aina moja).
Maambukizi ya awali ya tetekuwanga huweza kusababisha hali mbaya kwa mama na mtoto tumboni. Watu wakubwa huwa na hali mbaya zaidi kuliko watoto wadogo au vichanga kwa sababu huwa na kinga ya mwili ya juu sana inayoapambana na virusi hawa na kuleta madhara hayo. Hatari ya kupata nimonia kwa wamama walioathiriwa na tetekuwanga ni kubwa na huwa hatari kwa afya ya mama. Madhara kwa mtoto huweza kuwa, madhara ya uumbaji wa mifupa, macho, mfumo wa fahamu na figo. Kuna hatari kwa mtoto endapo maambukizi haya yametokea kati ya vipindi hivi viwili yaani wiki kati ya wiki ua 13 na 20 au wakati wakati wa kuzaliwa. Maambukizi katika kipindi cha miezi mitatu ya pili ya ujauzito huweza kusababisha mtoto kuzaliwa na matatizo ya kiuumbaji, maambukizi wakati wa kujifungua huweza kusababisha tetekuwanga kwa kichanga.
Mlipuko wa mkanda wa jeshi wakati wa ujauzito husababisha mama kutojihisi vema lakini si kitu cha hatari kwa mtoto, hata hivyo mama mwenye hatarishi ya kupata tetekuwanga endapo atakutana na mtu mwenye mkanda wa jeshi.
Je unaweza kuzuia maambukizi ya tetekuwanga?
Maambuikizi ya tetekuwaga yanaweza kuzuiwa kwa kinga inayotokea baada ya kupata maambukizi, au kwa kuchonjwa sindano ya kinga ya kirusi anayesababisha mkanda wa jeshi na tetekuwanga kwa wanawake walio na hatarishi ya kupata kirusi huyo. Sio tu kwamba mama atalindwa na adhara ya kirusi huyu bali hata kichanga naye atalindwa kutoka kwenye madhara ya kirusi ndani ya tumbo na wakati wa kuzaliwa.
​
Maambukizi ya CMV kwa mjamzito
​
Jinsi gani Kirusi CMV huathiri mtoto?
Maambukizi ya CMV hutokea mara kwa mara. Watu wazima wengi huwa na antibodi kwenye damu dhidi ya kirusi CMV zinazoonyesha kuwa walishaambukizwa na kirusi huyu kabla. Cha kusikitisha kuwepo kwa antibod hakumaanishi unalindwa kutopata maambukizi mengine yatakayotokea. Kwa sababu hakuna kinga na tabia ya pekee ya kirusi huyu, maambukizi wakati wa ujauzito hutokea si kwa nadra. Mama huwa hana dalili au anawezakuwa na dalili za wastani. Hata hivyo mtoto anaweza kuumwa dalili kali na kupata matatizo katika mfumo wa fahamu. Mtoto kutokuwa vema tumboni huweza kutokea kwa sababu ya maambukizi haya wakati mtoto yupo kwenye mfuko wa uzazi.
​
Maambukizi ya toxoplasma kwa mjamzito
​
Nini umuhimu wa kujua maambukizi ya toxoplamsa gondi wakati wa ujauzito?
Toxoplasma gondi ni kiini cha maradhi ambaye huambukizwa kwa njia ya kula nyama ilioambukizwa au kula chakula kilicho na kinyesi cha cha paka aliyeambukizwa. Kwa watu wenye kinga kamili ya mwili maambukizi hayana madhara. Kama mama mjamzito akipata maambukizi haya, maambukizi kwa mtoto hutokea. Maambukizi yanavyochelewa kutokea wakati wa ujauzito ndivyo yanavyowe kupenya na kuingia kwa mtoto. Kinyume nikwamba maambukizi yakitokea mapema wakati wa ujauzito ndivyo yanavyowezakusababisha madhara makubwa sana. Madhara kwa kichanga yanaweza kutoonekana au kuonekana kiasi au kusababisha maambukizi kwenye mifumo tofauti ya mwili kama mfumo wa fahamu. Kama maambukizi yametambuliwa kwenye kipindi cha kuhudhuria klinic basi yatatibiwa ili kuzuia madhara kwa kichanga.
Maambukizi ya awali kwa mama kabla ya ujauzito hujenga kinga ya kumlinda mtoto dhidi ya maambukizi mengine yatakayotokea. Mambo ya kawaida yanatakiwa kufanyika ili kuzuia maambukizi kwa mama.
Bonyeza hapa kusoma kuhusu Maambukizi ya streptococal
​
​
Imeboreshwa mara ya mwisho 07.07.2020
​
ULY Clinic inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchuku hatua yoyote ile inayohusu afya yako.
​
​​
Bonyeza kusoma makala zingine zaidi kuhusu;
​