USHAURI WA MATUMIZI YA DAWA KIPINDI CHA UJAUZITO NA KUNYONYESHA

Diphenhydramine na ujauzito
Taarifa kutoka kwa binadamu na wanyama zinatoa uzoefu wa kuwa diphenhydramine ni salama kutumika kwa wajawazito. Isipokuwa tafiti mmoja ambayo ilionyesha kuwa na mahusiano na mdomo sungura kwa mtoto mmoja aliyezaliwa na mama aliyetumia dawa hii wiki mbili kabla ya kujifungua. Kwa kuongezea matumizi kwenye muda wa wiki mbili kabla ya kujifungua kabla ya wakati wa ujauzito kufika, huhusiana na kuwa na hatari kubwa kusababisha madhaifu kwa kcihanga. Utafiti mmoja umependekeza kuwa dawa hii iwe chaguzi ya kwanza endapo kuna uhitaji wa kutumia dawa ya kuchoma kwenye mishipa jamii ya antihistamine

Meclizine na ujauzito
Meclizine ni piperazine aina ya antihistamine inayotumika sana kama dawa kichefuchefu na kutapika. Kwa ujumla dawa jamii ya antihistamine huchukuliwa kuwa na hatari kidogo za kusababisha madhara ya kiuumbaji kwa kichanga, hata hivyo, matumizi karibia na kujifungua kabla ya muda kufika huongeza hatari ya vichanga kuzaliwa na tatizo la kiuumbaji la fibroplasia ya retrolental

Promethazine na ujauzito
Promethazine ni antihistamine aina ya phenothiazine ambayo hutumika wakati mwingine kama dawa ya kuzuia kutapika au kupunguza maumivu wakati wa uchungu. Kuna ripoti kuhusu kutokea kwa madhara kwa kichanga lakini tafiti za kuthibitisha zinatakiwa kufanyika. Kwa ujumla, matumizi ya dawa hii wakati wa ujauzito huonekana kuwa na hatari kidogo ya kusababisha madhaifu ya kiuumbaji kwa kichanga.

Esomeprazole na ujauzito
Esomeprazole nidawa jamii ya Proton pump inhibitor (PPI).Kuna taarifa chache sana kuhusu matumizi ya dawa hii kwenye ujauzito, hata hivyo kuna tafiti moja inaonyesha kuwepo kwa uhusiano kati ya pumu ya kifua na aleji kwa watoto wanaozaliwa na mama aliyetumia dawa hii wakati wa ujauzito, hata hivyo tafiti hii inatakiwa kuthibitishwa.
Taarifa kutoka kwa wanyama na binadamu wajawazito zinaonyesha kuwepo kwa hatari kidogo ya madhaifu ya kiuumbaji kwa watumiaji wa dawa zingine jamii ya PPI, hata hivyo hatari ya matumizi ya esomeprazole haiwezi kuchunguzwa kiundani bila kuwa na taarifa zingine kutoka kwa watumiaji wa dawa hii kwenye ujauzito. Mpaka taarifa hizo zipatikane, kwa sasa ni vema kutumia dawa zingine jamii ya PPI endapo itahitajika wakati wa ujauzito kamalansoprazole au pantoprazole.

Loratadine na ujauzito
Hakuna ushahidi wa dawa hii kuongeza hatari ya madhaifu ya madhaifu ya kiuumbaji kwa kichanga endapo atatumia mama mjamzito. Uzoefu wa matumizi kwa binadamu wajawazito unatosha kuonyesha kuwa dawa hii si kihatarishi kikubwa cha kuwa sumu kwa kichanga. Endapo kutakuwa na ongezeko la vichanga wenye matatizo ya kiuumbaji, hii itakuwa si kawaida kwani mpaka sasa haijaonekana kuwa dawa jamii ya antihistamine huwa sumu kwa kcihanga.

Cetrizine na ujauzito
Cetrizine ni dawa ya antihistamine kizazi cha pili cha H1 receptor antagonist. Dawa hii haipo kwenye kundi la dawa zinazosababisha madhaifu ya maumbile kwa kijusi tumboni na hakuna taarifa za kutosha kuchunguza madhara kwa kijusi kwa binadamu wajawazito. Ingawa cetirizine inaonekana kuwa si sumu kwa kichanga, inapendekezwa kutumia dawa za kunywa jamii ya antihistamine daraja la kwanza kama
chlorpheniramine na tripelennamine, endapo kuna uhitaji wa kutumia dawa hii katika kipindi cha kwanza cha ujauzito. Cetirizine na loratadine zilikuwa zinakubalika kutumika kama mbadala wa chlorpheniramine na tripelennamine, isipokuwa katika kipindi cha kwanza cha ujauzito.
Levocetirizine na ujauzito
Hakuna ripoti zinazoelezea matumizi ya levocetirizine kwa binadamu mjamzito. Taarifa za wanyama zinaonyesha kuwepo kwa hatari kiasi, na hivyo kufanya kutowezekana kufahamu kuhusu madhara kwa ya kiuumbaji kwa kichanga. Hakuna taarifa zinazosema kwamba dawa jamii ya antihistamine pamoja na hii ni sumu ambayo inaweza pelekea kutokea kwa madhara ya kiuumbaji kwa kichanga tumboni. Licha ya hayo, endapo matumizi ya antihistamine yatahitajika wakati wa ujauzito, uchaguzi ni kutumia dawa zenye taarifa na zinappnekana kuwa afadhali zaidi kama vile chlorpheniramine au diphenhydramine.

Clarithromycin na ujauzito
Clarithromycin ni dawa inayofanana umbo na dawa zingine kundi la macrolide ambalo linahisisha dawa kama vile azithromycin, dirithromycin, erythromycin, na troleandomycin.
Tafiti za uzazi wa wanyama zinaonyesha zina hatari kubwa kudhuru uumbaji wa kichanga, hata hivyo taarifa za matumizi kwenye ujauzito zinatoa mapendekezo kwamba, hata kama hatari ipo kwa binadamu, hatarihiyo ni kidogo sana.



