top of page

Mwandishi:

Mhhariri

ULY CLINIC

ULY CLINIC

Imeboreshwa:

5 Aprili 2026, 05:10:33

Kichocho: Dalili, Visababishi, Vipimo na Matibabu

Kichocho: Dalili, Visababishi, Vipimo na Matibabu

Kichocho, ugonjwa unaofahamika kwa lugha ya tiba schistosomiasisi, ni ugonjwa unaofahamika kwa jina jingine la bilharzia. Ugonjwa huu husababishwa na minyoo na unaweza kuwa wa muda mfupi au au ugonjwa sugu.

 

Ugonjwa huu ni wa pili  kuathili au kuwapata watu katika bara la Afrika ikiongozwa na malaria. Ugonjwa wa kichoho umeonekana kutotiliwa umaanani katika ukanda huu wa jato.

​

Kimelea anayesababisha kichocho huishi kwenye maji yasiyo na chumvi na huishi ndani ya konokono. Kimelea anayesababisha kichocho anatengenezwa ndani ya konokono hufahamika kwa jina la serkaria huishi kwenye maji baada ya kutoka kwenye konokono,.

 

Mtu akiwa anaogelea haswa mida ya sa sita mchana, vimelea hawa hupenya kwenye ngozi ya mtu huyu  na kuingia katika mfumo wa damu. Maambukizi mengi ya kichocho hutokana na vimelea wanaoitwa Schistosoma (S) Mansoni, S.Hematobium na S.Japonicum 

 

Maambukizi yanatokeaje

Maambukizi  hutokea endapo mtu ataogelea kwenye maji yenye konokono wanaobeba vimelea vya kichocho, na endapo mtu aliyeambukizwa alijisaidia haja kubwa au ndogo kwenye maji hayo. Vimelea wanaowekwa na mtu aliyeambukizwa kwenye madimbwi ya maji husambaa kwenye maji hayo na  kuendeleza mzunguko wa maambukizi kwa watu wengine.

 

Mara baada ya mtu kumwaga mayai katika maji(wakati wa kujisaidia haja kubwa au ndogo), haya huingia kwa konokono na baadae hutotolewa na kuzalisha minyoo inayoitwa serkaria. Minyoo hii  hutoka nnje ya konokono na kuingia kwenye mwili wa binadamu kupitia ngozi.

 

Sekaria huweza kuishi mpaka masaa 48 baada ya kutoka ndani ya konokono na baadae hufa, mtu anaweza kupata maambukizi ya vimelea hawa endapo atakuwa anafua, kuoga, kuogelea au kuosha vyombo kwa maji yenye maambukizi ya vimelea hivyo.

 

Mara baada ya kuambukizwa, vimelea hukaa katika mishipa ya damu ili kukua na baada ya kukua hukutana kimwili na vimelea vya kike na kisha kutaga mayai. Mayai haya husafili kuelekea kwenye kibofu cha mkojo au matumbo/utumbo na kisha kutolewa kwa njia ya mkojo au kinyesi.

​

Dalili za kichocho

​Watu wengi huwa hawapati dalili mara baada ya kuambukizwa vimelea wa kichocho, hata hivyo dalili zinaweza kutokea ndani ya siku chache baada ya maambukizi hayo na huweza kuwa;

​

  • Kuwashwa ngozi au

  • Kupata vipele vinavyowasha

 

Ndani ya mwezi mmoja wa maambukizi, dalili za maambukizi huonekana ambazo zinaweza kuwa;

  • ​Homa,

  • Kutetemeka

  • Kukohoa na

  • Maumivu ya misuli

 

Dalili za kichocho hazitokani na maambukizi ya sekaria tu bali kutokana na kinga ya mwili kupambana na mayai ya vimelea hivi, hivyo kama mayai hayakutolewa nnje kwa njia ya mkojo au kinyesi, mayai haya hujishikiza kwenye kibofu na utumbo na kusababisha michomo(inflamesheni) na makovu kutokana na kinga ya mwili kushambulia mayai hayo.

 

Watoto wanaoambukizwa mara kwa mara ugonjwa huu hupelekea;

  • Kuishiwa  damu,

  • Kupata utapiamlo na

  • Kupata shida kujifunza kutokana na ugonjwa

 

Baada ya miaka kupita pia kichocho kinaweza kusababisha

  • Uharibifu kwenye matumbo,

  • Ini,

  • Bandama mapafu na

  • Kibofu

​

Kichocho pia kimeonekana kusababisha saratani ya  kibofu cha mkojo kwa watu wenye historia ya kuvua samaki, kulima mpunga, au umwagiliaji kwa kutumia maji baridi yaliyo na maambukizi ya kichocho.

​

Pasipo matibabu, kichocho kinaweza kuendelea kuwepo mwilini kwa miaka mingi.

 

Dalili za kichocho sugu

  • Maumivu ya tumbo,

  • Kuvimba kwa ini,

  • Kamu kwenye kinyesi au mkojo, na

  • Matatizo ya kupitisha mkojo na

  • Saratani ya kibofu cha mkojo,

 

Mara chache sana mayai yanaweza kuingia kwenye ubongo au uti wa mgongo na huweza kusababisha

  • Kupooza mwili

  • kifafa au

  • Michomo kwenye uti wa mgonjo unaosababisha magonjwa ya mfumo wa fahamu

 

Uchunguzi wa kimaabara

Uchunguzi wa kichocho hufanyika kwa kifaa cha kamera inayoweza kuona vimelea wadogo kwenye kinyesi na kuchunguza mayai ya vimelea hao. Mayai hayo huwa yanatolea kwa wingi au kwa kiwango kidogo mtu anapojisaidia haja, wakati mwingine vipimo vinaweza visione mayai hayo na kuhitaji kipimo cha damu kilicho kizuri zaidi kutambua maambukizi ya vimelea hao 

​

Matibabu

​Matibabu yapo kwa ajili ya kutibu kichocho cha mkojo na matumbo. Dawa aina ya praziquantel ambazo utaandikiwa na daktari wako hutumika kutibu maambukizi ya vimelea wa kichocho

​

Imeandikwa:

5 Aprili 2026, 05:08:50

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ya kitiba baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kubofya 'Pata Tiba,  au ''mawasiliano yetu' chini ya tovuti hii

bottom of page