Mwandishi:
Mhhariri
Dkt. Mangwella S, MD
Dkt. Salome A, MD
Alhamisi, 13 Julai 2023

Kufyonzwa kwa kichanga
Kufyonzwa kwa kichanga tumboni, ni mchakato unaohusisha umeng’enyaji wa kichanga aliyekufa, na ufyonzwaji wake kwenye mwili wa mama katika hatua yoyote ya ujauzito baada ya uumbaji wa ogani za mtoto kukamilika, yaani kuanzia wiki ya 9 na kuendelea kwa biandamu.
Mchakato huu ni wa asili na hufanywa na chembe za ulinzi wa mwili na hivyo huchukuliwa kuwa sehemu ya kawaida ya ujauzito. Kisababishi halisi bado hakifahamiki, ingawa kwa baadhi ya visa, huweza kuhusianishwa na hali au ugonjwa.
Mara baada ya kugunduliwa, daktari atafanya ufuatiliaji wa karibu kuchunguza kitendo cha ufyonzwaji ili kujihakikishia kwamba afya ya mama ipo kwenye usalama.
Visababishi
Kufyonzwa kwa kichanga kunaweza kusababishwa na sababu zinazofanya kichanga kufia tumboni zinazoweza kuhusisha;
Magonjwa na majeraha
Hali na magonjwa kwa mama na mtoto yanayoweza kupelekea kichanga kufa na kufyonzwa ni pamoja na;
Jeraha kwenye kizazi
Maambukizi kwenye kizazi
Madhaifu ya kiuumbaji
Matumizi ya dawa
Tafiti mbalimbali za wanyama zinaonyesha dawa zifuatazo zinasababisha kichanga aliye tumboni kufa hatimaye kufyonzwa
Diazoxide
Vitamin A kama ikizidi kiwango cha kawaida.
Thalidomide
Mycophenolate mofetil
Dawa zenye nguvu ya kuzuia utendaji kazi wa homoni estrogen kipindi cha kwanza cha ujauzito
Kemikali katika mazingira
Sumu ya kemikali zifuatazo zinaweza kupelekea ufyonzwaji wa kichanga ni kama zifuatazo"
Polychlorinated Biphenyls (PCBs) ambayo huweza kupatikana katika mazao mbalimbali yanayotumiwa na binadamu kama vile:
Dawa za kuua wadudu nyumbani na shambani
Rangi za nguo
Wino
Vyombo vya plastiki
Chupa za kulishia watoto
Mazao ya ujenzi kama grauti
Oili za magari, transfoma
Bulb za taa na maganda ya umeme
n.k
Upungufu wa vitamin na virutubisho
Katik tafiti za panya imeonyesha kuwa upungufu wa virutubisho vifuatavyo husababisha kkichanga kufia tumboni na kupelekea kichanga tumboni kufa na kufyonzwa:
Protini
Biotin
Pantothenic acid
Pteroylglutamic acid
Tocopherol
Riboflavin
Pyridoxine
Kufanyiwa upasuaji
Upasuaji wa kuondoa ovari kabla ya kutengenezwa kwa kondo la nyuma, hupelekea kuwa na upungufu wa homoni progesterone inayozalishwa na ovari.
Matibabu
Matibabu hulenga kuimarisha afya ya mama, na kama kuna mapacha, afya ya kichanga wa pili pia na wakati mwingine huhusisha kusitisha ujauzito kama hali ikionekana kuwa hatari.
Kinga
Kinga huhusisha kuejiepusha na kisababishi ambacho kinafahamika kama vile kutotumi dawa zinazofahamika kusababisha kichanga kufyonzwa kabla na wakati wa ujauzito.
Njia nyingine ni kuacha kuchafua mazingira kwa mazao na kemikali zinazofahamika kuwa sumu kwa binadamu haswa kwa kutumia njia bora ya kushughulika na mabakia ya mazao hayo sumu.
Wajawazito wanashauriwa kutumia vitamin A kutoka kwenye vyanzo asili na katika kiwango kinachoshauriwa kiafya.
Unaweza kusoma pia kuhusu
Kupotea kwa mimba
Kupotea kwa ujauzito
Kufyonzwa kwa kijusi
Kuyeyuka kwa pacha
Kupotea kwa ujauzito tumboni